Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

WAKURUGNZI Watendaji saba wa kampuni tano za jijini Dar es Salaam wanatarajia kupanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Februari 23 na Machi 12, mwaka huu.

Imeelezwa Wakurugenzi hao ambao walitakiwa kusomewa mashtaka yao leo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi ni, lakini ilishindikana kwa kuwa hawakuwepo ni Omari Mgwaya na Nelson Rubagumisa wa kampuni ya Panacom Solution Co.Ltd, Issa Lupigila wa kampuni ya Upame Co.Ltd na  Osca Chongola wa kampuni ya Nolc Engineering Company, 

Wengine ni,Petronia Mrosso na Fritz Masanjo wa Kampuni ya Skyscape International Co.Ltd, na Josephat Mwita wa kampuni ya Tan Geo Info Consult,

Washtakiwa  hao wanakabiliwa na kesi za jinai namba 38, 31, 37, 39 na 32 zote za mwaka 2018, 

Katika kesi inayomkabili Osca, Wakili wa Serikali Dereck Mukabatunzi alidai kesi ilipangwa kwa ajili ya mshtakiwa hiyo kusomewa mashtaka yanayomkabili.

Wakili wa mshtakiwa,Hassan Kihangio aliieleza mahakama kuwa mteja wake ni mgonjwa, anamatatizo katika pingili za uti wa mgongo, yupo hospitali amepewa mapumziko akaomba apangiwe tarehe nyingine ili afike asomewe mashtaka.

Kutokana na suala la ugonjwa upande wa mashtaka haukuwa na pingamizi na Hakimu Nongwa amahirisha kesi hiyo hadi Machi 12, 2018.

Naye Wakili wa Serikali Emmil Kilia aliyetakiwa kumsomea mashtaka Issa Lupagila alidai kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya mshtakiwa huyo kusomewa mashtaka yanayomkabili lakini hawakuweza kumpata ili wampatie wito wa mahakama afike mahakamani hivyo wakaomba hati nyingine ya mwito.

Kilia amedai wanaendelea kumtafuta baada ya kueleza hayo Hakimu Nongwa aliamuru wapewe hati ya wito na kesi imeahirishwa hadi Machi 12,2018 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama atakuwa amepatikana ama la.

Katika kesi inayomkabili Joseph Mwita, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Benson Mangowi alieleza mahakamani hapo kuwa mshtakiwa huyo hawajaweza kumpata hivyo aliiomba mahakama itoe hati ya wito ili waweze kumpata na kumsomea mashtaka yanayomkabili.

Kesi imeahirishwa hadi Machi 12,mwaka 2018.

Katika kesi inayomkabili Omari Mgwaya na Nelson Rubagumisa, Wakili wa Serikali,Emma Msofe aliieleza Mahakama  washtakiwa hao hawajaweza kuwapata ili kuwapatia hati ya wito wa mahakama.

Hivyo aliiomba wapatie hati ya mwito nyingine ili waweze kuwapatia washtakiwa hao wafike mahakamani kusomewa mashtaka yanayowakabili.Kesi imeahirishwa hadi Machi 12,mwaka 2018.

Katika kesi inayowakabili, Petronia Mrosso na Fritz Masanjo, Wakili was Serikali, Dereck Mukabatunzi alieleza washtakiwa walipokea hati ya mwito wa mahakama ila wapo nje ya mkoa wa Dar es Salaam.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 23, mwaka 2018 ambapo washtakiwa hao watasomewa mashtaka yanayowakabili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...