Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akimsikiliza kwa makini Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Georgia Mutagahywa (kulia) muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya utiaji saini mikataba ya usambazaji huduma za mawasiliano ya simu za mkononi maeneo ya vijijini kati ya makampuni ya simu na Mfuko wa Wamasiliano kwa Wote - (UCSAF) jijini Dar es salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasilano wa Airtel Beatrice Bandawe.
Mkuu wa Idara ya Sheria wa Vodacom Ngayama Matongo akimuongoza Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo Georgia Mutagahywa (aliyeketi) kutia saini mkataba wa makabaliano ya usambazaji huduma za mawasiliano vijijini kupitia ruzuku ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam. Wa pili kulia aliyesimama ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof Makame Mbarawa akishuhudia. Vodacom kupitia mfuko huo itafikisha huduma kwenye kata 37 za pembezoni mwa miji na yenywe ikiahidi kufikisha huduma kwenye kata 36 za pembezoni kwa gharama zake ili kuwawezesha watanzania wasihia vijijini kuunganishwa kwenye mtandao wa huduma za simu za mkononi.
Kutoka kulia Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Georgia Mutagahywa, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Kamugisha Kazaura na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Peter Ulanga wakitia saini makubaliano yanayayawezesha makampuni ya simu kupokea ruzuku kwa ajili ya kufikisha huduma kwenye maeneo yaliyo pemebezoni na miji kadiri walivyoomba. Vodacom imeahidi kufikisha huduma hiyo kwenye kata 73 kati ya hizo 37 kupitia ruzuku YA UCSAF.
Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Georgia Mutagahywa kulia akibadilishana nyaraka za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Kamugisha Kazaura zinazohusiha upokeaji wa ruzuku kwa ajili ya kufikisha huduma za mawasiliano vijijini inayotolewa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).Wa kwanza kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo Peter Ulanga akisainia makubaliano hayo. Vodacom imeahidi kufikisha huduma kwenye kata 73 zilizopo vijijini kati ya hizo 37 kupitia ruzuku hiyo. Wa pili kulia waliosimama ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof Makame Mbarawa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...