Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Mkoani Manyara Jitu Vrajlal Son, akiwakabidhi kompyuta Makamu Mkuu wa shule ya sekondari Chief Dodo ya Kata ya Riroda Jackson Warae na Mratibu elimu kata ya Riroda Peter Yaghambe, mbunge huyo aligawa kompyuta tano kwenye tarafa ya Goroi ambapo kila shule ya sekondari kwenye kata tano za tarafa hiyo zilipata kompyuta moja, katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Nicodemus Tarmo.
Mafundi wakiziweka sawa baiskeli 32 za wahudumu wa afya vijijini zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Mkoani Manyara Jitu Vrajlal Son, kwa ajili ya wahudumu 32 wa afya wa vijiji vya Tarafa ya Goroi.
Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Mkoa wa Manyara Jitu Vrajlal Son, akimkabidhi baiskeli Yustine Naamo mmoja kati ya wahudumu wa afya vijijini wa Kijiji cha Riroda, kati ya baiskeli 36 alizozigawa kwa wahudumu 36 wa afya vijiji vya Tarafa ya Goroi.
Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Mkoani Manyara Jitu Vrajlal Son, akisalimiana na baadhi ya wahudumu wa afya vijijini wa vijiji vya Tarafa ya Godoi baada ya kukabidhi baiskeli 36 kwa wahudumu hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...