Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu jijini Arusha wanatarajiwa kujengewa Hostel zitakazowasaidia kuondokana na adha ya kupata
sehemu za malazi hivyo kulazimika kulala maeneo ya stendi za mabasi na
masoko.
Mkurugenzi wa shirika la Gola
linalojihusisha na masuala ya
watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu jijini Arusha,Sawale Maghema amesema kuwa
mpango huo utasaidia watoto hao kuondokana na mazingira magumu yanayowapelekea kujiingiza katika
vitendo vya uhalifu na matumizi ya madawa ya kulevya.
Sawale alisema kuwa iwapo watoto hao watatelekezwa na
jamii bila kusaidiwa wanaweza kugeuka na kuwa mwiba kwa jamii ya Watanzania
hivyo amewataka Watanzania kujitokeza kuwasaidia watoto hao .
"Watoto hawa tuna mpango
maalumu wa kuwakusanya na
kuwakutanisha pamoja kujua mahitaji yao ,malengo na matarajio waliyonayo ili
kuwasaidia kwa kushirikiana na jamii hata kwa hili la ujenzi wa Hostel
litasaidia kuwaweka pamoja tukiwaacha waendelee kukaa mitaani hawatabadilika
wataendelea kuwa na maisha mabaya" Alisema Sawale
Mdau wa Masuala ya utalii Mustafa
Panju alijitolea kuwasaidia watoto hao kwa
kuchangia kiasi cha shilingi milioni 20 ili waweze kupata
mahitaji muhimu ,Ameeleza kuwa jamii
inapaswa kuamka na kuwasaidia watoto hao badala ya kuwaacha waendelee kukaa
kwenye mazingira hatarishi.
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto
Arusha ,Hassan Omari
akizungumza kwa niaba ya watoto wa mitaani anaeleza kuwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wana
ndoto nyingi,vipaji na uwezo wa hali ya juu hivyo wakisaidia wanaweza kufika
mbali na kulisaidia taifa .
Chanzo:libeneke la kaskazini blog
Kikundi cha ngoma cha watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wakitumbuiza katika shughuli ya kuwakusanya watoto wa mitaani iliyofanywa na taasisi ya GOLA Foundation inayolenga kuwasaidia watoto hao kukabiliana na changamoto za ukosefu wa malazi,chakula,mavazi na pia elimu.Jamii inaombwa kujitokeza kusaidia watoto hao
Baadhi ya Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu jijini Arusha waliokusanywa na taasisi ya GOLA Foundation inayolenga kuwasaidia watoto hao kukabiliana na changamoto za ukosefu wa malazi,chakula,mavazi na pia elimu.Jamii inaombwa kujitokeza kusaidia watoto hao
Chanzo:libeneke la kaskazini blog
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...