Waziri wa zamani Daniel Yona akiituliza familia yake mara baada ya hukumu kutolewa leo katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es salaam.
Waziri wa zamani Basi Mramba akiteta na mawakili wake baada ya kuhukumiwa leo mahakamani Kisutu.


Mawaziri wa zamani Basil Mramba  na Daniel Yona  leo wamekutwa na hatia na katika kesi iliyokuwa inawakabili kifungo cha kwenda jela miaka mitatu kila mmoja kwa kukutwa na makosa 10 ya matumizi mabaya ya madaraka. 

 Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi Grey Mngonja (kushoto)  ameachiwa huru bada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha makosa dhidi yake. 

Pia Mahakama hiyo imewahukumu kulipa faini ya shilingi milioni 5  au kwenda jela miaka 2 zaidi baada ya kukutwa na hatia ya kuisababishia serikali hasara ya shilini bilioni 11.7. 

Washitakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 11.7 kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni iliyopata zabuni ya ukaguzi wa madini ya dhahabu nchini.
Hukumu hiyo imetolewa chini ya jopo la mahakimu watatu ambao ni Hakimu Saul Kinemela, Jaji Sam Rumanyika na Jaji John Utamwa aliyekuwa mwenyekiti wa jopo hilo baada ya kupitia ushahidi pamoja na vielelezo vilivyowasilishwa na pande zote mbili katika kesi hiyo.
Kwa mara ya kwanza washitakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo mwaka 2008 wakikabiliwa na mashitaka ya kuisababishia serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya kukagua madini ya dhahabu ya M/S Alex Stewart ya Uingereza.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Bibi UmemeJuly 06, 2015

    kweli sharia ni msumeno, ila hilo la kuachiwa Papaa Msofe linanitatiza akili

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 06, 2015

    Vipi kuhusu hukumu ya kuchapwa viboko pia

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 06, 2015

    hukumu ya mabilioni miaka mitatu tu na huko jela kutakuwa na upendelea wa kufa mtu.tanzania aliyeiloga alikufa

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 06, 2015

    mbona hukumu ndogo sana kial Maranda na Farijala wamekula mitano mitano ,wwao walikula million 200 tu sasa hao wa mabilion miaka mtatu tu?

    Mimi sielewi

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 07, 2015

    Yaani kesi yaendeshwa kwa miaka saba kisha mtu anafungwa miaka mitatu jela na faini ya milioni tatu tu!Walau kajala alilipa milioni 13 na kuepuka kifungo kirefu ambapo aliekua mumewe anatumikia zaidi ya miaka 10 jela kwa kesi ndoogo.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 07, 2015

    Mungi ibariki nji yetu

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 07, 2015

    Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 07, 2015

    Mimi nilitegemea miaka 30 jela, kurudisha hayo mabilioni na viboko juu. Hapo mnawaambia na wengine wenye mawazo kama hayo bongo hakuna matata

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 07, 2015

    Nikweli kifungu kidogo lkn tumepiga hatua kubwa .
    Kuweza kumfunga mtu alie kuwa waziri nijambo kubwa na lakupongezwa sasa wengine kabla ya kufanya makosa watajishauri marambilimbili.
    Mini ninaona tuipongeze serikali na tuipongeze Mahakama yetu kwa hatua kubwa walio piga hii.

    Inaonekana tunakokwenda ni kuzuri kumbe minyangumu pia inaweza kufungwa.

    ReplyDelete
  10. movie ndo kwanza imeanza sterling ni mranba.. za kuambiwa changanya na za kwako...JMK

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 07, 2015

    MAHAKAMA IEPUKE DOUBLE STANDARD.KOSA DOGO LINAKUWA NA HUKUMU KUBWA,INAKUWAJE KOSA LA MABILIONI WATU WAHUKUMIWE MIAKA MITATU TU

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 07, 2015

    MIE NAONA WANGEFILISIWA MALI ZAO KUFIDIA PESA WALIZOIBA ILI IWE FUNDISHO KWA VIGOGO WENGINE, AU NANI ATALIPA HIZO BILIONI 11

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...