MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA UNAPENDA KUWATANGAZIA WANACHAMA NA WANUFAIKA WOTE KWAMBA KATIKA KUBORESHA HUDUMA KWA WANACHAMA WAKE, HUDUMA ZA VIBALI MAALUM VYA MATIBABU ZILIZOKUWA ZINATOLEWA KATIKA OFISI ZA MAKAO MAKUU YA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA, ILIYO KURASINI BENDERA TATU HAZITATOLEWA TENA OFISI HII ISIPOKUWA KWA WAGONJWA WAPYA WANAOHITAJI VIBALI VYA DAWA ZA SARATANI  HUDUMA ZA KUSAFISHA FIGO (DIALYSIS) NA DAWA ZA KUDHIBITI NA KUONGEZA  KINGA KWA WALIOWEKEWA FIGO PANDIKIZI.

KWA WANACHAMA WALIOKWISHA ANZA KUPATA HUDUMA ZA VIBALI, WATAPATA HUDUMA HIZO KATIKA OFISI ZA NHIF ZA MIKOA NA BAADHI YA HOSPITALI KAMA IFUATAVYO:-

·      DAR ES SALAAM: HOSPITALI YA MUHIMBILI, MOI, OCEAN ROAD, BESTA, REGENCY NA TMJ, OFISI YA NHIF ILALA (JENGO LA USHIRIKA-GHOROFA NA.15), KINONDONI (JOSAM HOUSE GHOROFA YA. 4) NA TEMEKE (MKABALA NA HOSPITALI YA TEMEKE).

·      KWA MIKOA MINGINE VITUO VILIVYOWEZESHWA KUTOA HUDUMA HIZI NI KCMC (MOSHI), ALMC (ARUSHA), HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA – MBEYA. ZOEZI LINAENDELEA KUWEZESHA VITUO VINGINE NA TAARIFA ZITATOLEWA.

HUDUMA ZINAZAZOTELEWA VIBALI KATIKA VITUO HIVYO NI:-
CT SCAN, MRI, HUDUMA ZA KUSAFISHA FIGO (DIALYSIS), DAWA ZA SARATANI, VIFAA SAIDIZI, DAWA ZA KUDHIBITI NA KUONGEZA KINGA KWA WALIOWEKEWA FIGO PANDIKIZI, MIWANI YA KUSOMEA NA NYONGA AU GOTI BANDIA.

MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA UNAOMBA RADHI KWA USUMBUFU WOWOTE UTAKAOJITOKEZA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MABADILIKO.
UKISIKIA/KUSOMA TANGAZO HILI TAFADHALI MWARIFU NA MWENZAKO.


LIMETOLEWA NA KAIMU MKURUGENZI MKUU -NHIF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...