Mwenyekiti wa Jukwaa Huru la Wazalendo Ndugu Salum Ally Hapi akizungumza na waandishi wa habari kwenye hotel ya Travetine ,Magomeni jijini Dar es Salaam, kulia ni Katibu wa Jukwaa hilo Ndugu Mtela Mwampamba.

Ndugu wanahabari,

Mbele yenu sisi tuliowaita hapa ni Jukwaa Huru la Wazalendo ambalo limeitisha mkutano huu ili kufikisha yale tuliyoyakusudia kuwaeleza umma wa watanzania.

Sote tunatambua kuwa nchi yetu imetoka katika uchaguzi mkuu ambao umetupatia viongozi wapya wa awamu ya tano ya uongozi wa taifa letu chini ya Dr. John Pombe Joseph Magufuli. Tunapenda kuwapongeza watanzania wote kwa uchaguzi wa amani na utulivu. Aidha kwakua ndio mara yetu ya kwanza kuzungumza nanyi tunapenda kuwapongeza wanahabari wote kwa kazi nzuri ambayo mmekua mkiifanya kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu nchini. Tunawashukuru sana.

Mkutano wetu huu umebeba madhumuni makubwa mawili.

Kwanza ni kumpongeza Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hotuba yake aliyoitoa Bungeni siku ya ufunguzi wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 19/11/2015. 

Tunaiunga mkono Hotuba yake ambayo kwa kweli ilikuwa imebeba Uzalendo, Ujasiri, dira ya kweli ya maendeleo ya taifa letu na muuelekeo mpya wa Serikali ya awamu ya tano. Mambo yote aliyozungumzia Mh. Rais yamebeba maslahi mapana ya nchi yetu na yanalenga kuijenga Tanzania mpya ambayo waasisi wa Taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Abeid Amani Karume walikusudia kuijenga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Tafuteni kazi ya maana ya kufanya. Kila mtu akiunda kikundi cha kumpongeza rais italeta tija gani katika uzalishaji?

    ReplyDelete
    Replies
    1. MAANKA MAYRANovember 26, 2015

      HIKI KIKUNDI HAKIKUUNDWA KWA AJILI KIMPONGEZE RAIS HIKI KIKUNDI KIPO SIKU ZOTE NI KWAMBA KIMEJITOKEZA TU KUTOA PONGEZI, NA HIZO ZIMETOLEWA NYINGI TU KUTOKA SEHEMU MBALI MBALI NA SIO HICHO CHA WAZALENDO TU. NA TIJA IPO MAANA HII NI KWAMBA TUNAMPA NGUVU RAIS KUFANYA KAZI YAKE KWA FAIDA YA TAIFA NA WATZ WOOTE. HAPA NAONA KUNA KIASHIRIA CHA KISIASA HAPA, JAMANI UCHAGUZI UMEKWISHA RAIS NI MAGUFULI NA AMEANZA KWA KULETA MAGEUZI AMBAYO WATZ WOOTE TUKIYAPIGANIA. MIMI NI MWANA CUF DAMU, UKWELI USEMWE MAGMAG NIMEMKUBALI NI JEMBE. TUMUUNGE MKONO KWA MANUFAA YA TAIFA.

      Delete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...