Mnamo Mei mwaka huu, shirika la ndege la la Etihad linategemea kufungua sehemu mpya ya mapumziko katika stesheni ya tatu ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi kwa ajili ya wageni wake wa “Daraja la Kwanza”, wasafiri wenye kadi maalum za Platinum za Etihad, wasafiri wenye kadi maalum za Platinum kutoka washirika wa Etihad na wale watakaotumia huduma ya “Makazi” iliyopo katika ndege zake aina ya Airbus A380. Etihad imewekeza sana katika kutimiza lengo hili kwa ajili ya wageni wake wa hadhi ya juu wanaopenda huduma zenye viwango bora zaidi.

Peter Baumgartner, Afisa Mkuu wa Biashara, alisema: “Huduma hii itakuwa kito katika taji letu hapa Abu Dhabi, ni nafasi nzuri kuonesha umahiri wetu kwenye ubunifu na uvumbuzi. Ni muhimu kwetu kuhakikisha msafiri anapata huduma bora kwanzia uwanjani hadi angani mpaka anaposhuka. Tuna imani huduma na bidhaa tutakazotoa nje ya ndege zitajizolea umaarufu kama za ndani ya ndege na tunategemea wateja watafurahia yote tunayowaandalia.”

Sehemu hii ya mapumziko itapambwa kwa mtindo wa Kiarabu na itaendana na umaridadi na umahiri uliozoeleka na kuhusishwa na jina la Etihad. Sehemu hii itaonesha uzoefu na ustadi wa Etihad na jinsi walivyojikita katika kuleta huduma yenye ukamilifu, kuanzia angani hadi ardhini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...