Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Makao Makuu tarehe 12/2/2016 imewafikisha washtakiwa wafuatao mahakamani, ambao pia ni maafisa waandamizi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL):
1. Kipalo Amani Kisamfu, Mkurugenzi Mkuu wa TRL
2. Jaspar hurbert Kisiraga, Mhasibu Mkuu wa TRL
3. Mathias Andrew Massae
4. Muungano Gabriel Kaupunda
5. Ngoso Joseph Mwakilembe Ngosomwiles
6. Pascal John Mafikiri
7. Kedmon Peter Mapunda
8. Felix Rwezaula Kashaigili
9. Lowland Watson Simtengu
10. Josepth Mlinda Syaizyagi
11. Charles Florence Ndenge

Washitakiwa hawa wakiwa Maafisa Watendaji Wakuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) wanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya na kutumia nyaraka kumdanganya Mwajiri kinyume na kifungu cha 22 na 31 vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Kwa nyakati tofauti washitakiwa wanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya na nyaraka kwa kuipatia zabuni Kampuni ya HINDUSTHAN ENGINEERING AND INDUSTRIES ambayo haikukidhi vigezo, kuleta mabehewa ya kokoto nchini.
Fedha ambazo zimeshalipwa kwa Kampuni ya HINDUSTHAN ni dola za kimarekani 1,280,593.75 kati ya dola 2,561,187.50

Washtakiwa wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kufunguliwa kesi namba 49/2016 inayosimamiwa na Mhe. Hakimu Mchaura. Kesi imepangwa kusikilizwa tarehe 25/2/2016.

IMETOLEWA NA OFISI YA AFISA UHUSIANO
TAKUKURU, MAKAO MAKUU
12February 2016


 Viongozi wa Kampuni ya Shirika la Reli nchini Tanzania (TRL), wakiwafikishwa  katika  mahakama ya  Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Dalaam tayari kwa kusomewa mashitaka 9 yanayowakabili likiwemo la  tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka. 

Viongozi wa wa Kampuni ya Reli nchini Tanzania (TRL), wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam kusomewa mashitaka 9 yanayowakabili likiwemo la  tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka, wa pili kulia ni aliyekuwa Mkurugenzi wa shirika hilo,  Mhandisi Kapallo Kisamfu. 
PICHA ZOTE NA KHAMIS MUSSA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. The mdudu, tupa lupango mikubwa mizima lakini haina hata machungu na nchi yao hao ni #mamrukiii

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...