Waziri wa Nishati na
Madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Profesa Sospeter
Muhongo amezindua Mafunzo ya namna ya
Kutengeneneza Taa na Chaja zinazotumia mwanga wa jua kwa vijana 20 katika Kata ya Nyegina Mkoa wa Mara.
Akifungua mafuzo hayo
Profesa Muhongo amewataka vijana hao kuwa mabalozi wazuri wakati wanapohudhuria
mafunzo na kueleza kuwa, yatakuwa chachu katika kupanua wigo wa wa ajira ikiwemo wahitimu kujiari wenyewe.
Profesa Muhongo
amewataka vijana na wananchi mkoani humo kuweka nguvu kubwa katika elimu
kutokana na umuhimu na mchango wake kwa
maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Akizungumzia kuhusu
Mradi wa Usambazaji Vijijini Awamu ya Tatu, Profesa Muhongo ameeleza kuwa,
awamu hiyo itaanza kutekelezwa kuanzia mwezi Machi mwaka huu na kuongeza kuwa,
mradi huo utafanywa kwa Awamu na kusisitisza kuwa, adhma ya Serikali ni
kuhakikisha kuwa, ndani ya kipindi cha miaka mitano vijiji vyote nchini viwe
vimeunganishwa na nishati hiyo.
" Vijiji vyote
vitaunganishwa na nishati ya umeme. Tutasambaza
awamu kwa awamu na lengo letu ni kuhakikisha kuwa, vijiji vyote chini
vinaunganishwa na umeme ndani ya kipindi cha miaka mitano. Wale ambao
hawajafikiwa awamu ya kwanza na ya pili tutawafikia awamu ya tatu vivyo hivyo
mpaka tufikie lengo letu," amesisitiza Prof. Muhongo.
Kwa upande wake
Balozi wa Korea Kusini nchini, Song Geumyoung ambaye nchi yake imefadhili
mafunzo hayo, amesema kuwa, uwepo wa taa
hizo utasaidia upungufu wa umeme hususan maeneo ya vijijini na ambayo bado
hayajaunganishwa na nishati hiyo.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akionesha mfano wa Taa zinazotumia mionzi ya jua ambazo vijana 20 katika Kata ya Nyegina watafundishwa namna ya kuzitengeneza baada ya kuzindua mafunzo hayo. Kulia ni Balozi wa Korea Kusini nchini, Song Geumyoung na kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo hayo Dkt. Hong- Kyu Choi.
Mkufunzi wa mafunzo ya kutengeneza Taa na Chaja zinazotumia mionzi ya jua, Dkt. Dkt. Hong- Kyu Choi, akiwaleza washiriki wa mafunzo namna mafunzo hayo yatakavyoendeshwa.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma Vijijini, Dkt. Vicent Naano, (wa tatu kushoto) akiongea jambo mara baada ya uzinduzi wa mafunzo ya Kutengeneza taa na chaja zinazotumia mionzi ya jua. Wengine ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muongo (katikati), Balozi wa Korea Kusini nchini,Song Geumyoung Mkufunzi wa mafunzo hayo Dkt. Hong- Kyu Choi (wa pili kulia) na baadhi ya wawakilishi wa vijana wanaoshiriki mafunzo.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akiweka tofali katika moja ya vyumba vya madarasa vinavyojengwa katika Shule ya Msingi Kata ya Bwasi, wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa shuleni hapo. Wengine ni Viongozi wa Vijiji, Halmashauri na wananchi wa Kijiji cha Kome.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...