Na Ismail Ngayonga .

MAAFISA Habari na Mawasiliano Serikalini katika Mikoa na Halmashauri nchini wametakiwa kutumia njia za haraka na za kisasa katika mawasiliano ikiwemo matumizi ya tovuti na mitandao ya kijamii ili kutangaza shughuli na mafanikio ya sera na mipango ya Serikali kwa wananchi.

Hayo yamesemwa jana Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas wakati wa uzinduzi wa tovuti za halmashauri 35 za mikoa 5 ya kanda ya ziwa inayojumuisha Mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga na Simiyu.

Dkt. Abbas alisema pamoja na kuwepo kwa vyombo mbalimbali vya habari vinavyotumika kufikisha taarifa za habari kwa wananchi ikiwemo magazeti na redio, bado mitandao mitandao ya kijamii ikiwemo barua pepe imendelea kutumia na wananchi wengi zaidi ulimwenguni kwa sasa. 

“Kwa sasa nusu ya watu duniani wapo mtandaoni na hapa nchini kwa mujibu wa ripoti ya TCRA (Mamlaka ya Mawasiliano Nchini) inaonyesha kuwa Watanzania zaidi ya Milioni 19 wapo mtandaoni aidha kwa kutumia barua pepe au kutembelea kurasa za facebook” alisema Dkt. Abbas.

Kwa mujibu wa Dkt. Abbas alisema sifa za Afisa Habari na Mawasiliano wa karne ya sasa ni mwenye uwezo wa kutumia njia za kisasa za mawasiliano, ambazo zitamwezesha kujibu hoja mbalimbali kwa haraka zaidi badala ya kusubiri Serikali kulalamikiwa na wananchi.

Aidha Dkt. Abbas alisema uzinduzi wa tovuti katika mikoa na halmshauri hizo ni kigezo muhimu kitakachotumiwa na Serikali katika kupima wa utendaji kazi wa Maafisa Habari katika kushughulikia kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Akifafanua zaidi Dkt. Abbas alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa tovuti za mikoa na halmashauri za Wilaya nchini zinaendelea kuwa hai na zenye taarifa zilizozingatia muda na wakati na hilo litawezekana iwapo Maafisa Habari watatimiza malengo wanayopaswa kujiwekea katika maeneo yao ya kazi.
 Mkurugenzi wa Habari na  Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas akizungumza na Maafisa Habari na Tehama wakati wa Mafunzo elekezi ya matumizi ya tovuti kutoka Mikoa 5 na Halmashauri 35 za Mikoa ya Kanda ya Ziwa  yaliyofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekaani (USAID) na kusimamiwa na Ofisi ya      Rais- TAMISEMI,  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wakala ya Serikali Mtandao (EGA). Mafunzo hayo yalianza tarehe 9-20 Februari, 2017, kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Rebecca Kwandu. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...