Maelfu ya waombolezaji leo wamehudhuria mazishi ya aliyekuwa Meya wa jiji la Dar es salaam marehemu Kleist Sykes aliyezikwa leo Alhamisi Novemba 23, 2017 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.

Viongozi mbalimbali walihudhuria mazishi hayo ya Marehemu Kleist Sykes, aliyefariki dunia jana Jumatano Novemba 21, 2017, wakiwemo Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa aliemuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Marehemu  Kleist Sykes, ambaye alikuwa mtoto wa marehemu Abdulwahid Sykes, mmoja wa waasisi wa chama cha TANU, na ambaye alipewa jina la babu yake Mzee Kleist Sykes, alikuwa Meya wa jiji la Dar es salaam na pia diwani wa kata ya Kivukoni kati ya mwaka 2000 na 2005. Pia alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
 Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Meya wa jiji la Dar es salaam marehemu Kleist Sykes likiwasili katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam leo Novemba 23, 2017 
Abraham Sykes, mdogo wa  aliyekuwa Meya wa jiji la Dar es salaam marehemu Kleist Sykes akiweka udongo kaburini katika  makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam leo Novemba 23, 2017 
 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika mazishi ya aliyekuwa Meya wa jiji la Dar es salaam marehemu Kleist Sykes  katika  makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam leo Novemba 23, 2017 
 Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa aliemuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli akishiriki katika mazishi ya aliyekuwa Meya wa jiji la Dar es salaam marehemu Kleist Sykes  katika  makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam leo Novemba 23, 2017 
 Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman  akishiriki katika mazishi ya aliyekuwa Meya wa jiji la Dar es salaam marehemu Kleist Sykes  katika  makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam leo Novemba 23, 2017 
 Msanii Dully Sykes akishiriki katika mazishi ya baba yake mkubwa aliyekuwa Meya wa jiji la Dar es salaam marehemu Kleist Sykes  katika  makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam leo Novemba 23, 2017 
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa aliemuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Mzee Kingunge Ngombare Mwilu na Mtahiki Meya wa Manispaa wa Kinondoni Mh.Benjamin Sitta wakiwa mazishini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...