Na Beatrice Lyimo- Maelezo, Dodoma
Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amewataka viongozi mbalimbali wa mahakama ikiwemo Naibu Wasajili, Mahakimu, Watendaji, Wakuu wa Idara na Vitengo kutenda haki kwa watumishi walio chini yao.
Jaji Mkuu ameyasema hayo leo Mkoani Dodoma wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa baraza la wafanyakazi wa mahakama Tanzania.
“Sisi kama wasimamizi wakuu wa haki nchini tunawajibu mkuu wa kutenda haki kwa watumishi kwa vitendo, ni ukweli usiopingika kwamba kimbilio la mtumishi yeyote aliyefikwa na matatizo ni kwa kongozi wake katika sehemu yake ya kazi, hivyo basi kila kiongozi anapaswa kufungua milango kwa watumishi waliopo chini yake” amesema Jaji Mkuu.
Jaji Mkuu ameongeza kuwa, ubora wa viongozi unapimwa kwa namna wanavyosaidia wafanyakazi walio chini yao, hivyo kuwataka viongozi hao kutokufunga milango yao kwa watumishi wanaowaongoza.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akihutubia Baraza la Wafanyakazi wa  Mahakama  ya Tanzania leo Jijini Dodoma.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof.  Ibrahim Juma (katikati) akishiriki kuimba wimbo wa mshikamano kabla ya kufungua  Baraza la Wafanyakazi wa  Mahakama ya Tanzania leo Jijini Dodoma.
 Wajumbe wa menejimenti ya Mahakama ya Tanzania wakishiriki kuimba wimbo wa mshikamano wakati wa kikao cha Baraza la wafanyakazi leo Jijini Dodoma.
 Sehemu ya washiriki  wa Kikao cha Baraza la wafanyakazi kutoka Kanda ya  Dar es Salaam wakifuatilia kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania leo Jijini Dodoma.
 Wajumbe wa Kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi ambaye ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.  Prof. Ibrahim Juma.
 Wajumbe wa Menejimenti  ya Mahakama ya Tanzania wakifuatilia hotuba ya Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma  wakati wa Kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania .
 Katibu wa Baraza la Wafanyakazi  Mahakama ya  Tanzania Bibi Rose  Tengu akitoa maelezo ya awali kuhusu  Baraza la Wafanyakazi wa  Mahakama Tanzania leo Jijini Dodoma.
(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...